Feitoto aubeba uchezaji bora wa Mwezi
Eric Buyanza
December 5, 2023
Share :
Kamati ya tuzo za TFF imemchagua kiungo mshambuliaji wa Azam Fc, Feisal Salum kuwa mchezaji bora wa mwezi Novemba wa ligi kuu ya NBC 2023/24, huku Bruno Ferry, kocha wa Azam Fc akichaguliwa kuwa kocha bora wa ligi kuu ya NBC kwa mwezi huo.
Fei ambaye amehusika na mabao 6, akifunga mawili na kupika manne katika dakika 254 za michezo mitatu aliyocheza, amewashinda Kipre Junior wa Azam Fc na Mx Nzengeli wa Yanga walioingia fainali kwenye mchakato wa Tuzo hizo.
Bruno aliiongoza Azam kushinda michezo mitatu iliyocheza kwa mwezi huo, ikifunga mabao 11 na kufungwa bao 1 huku ikipanda kutoka nafasi ya 4 hadi ya 2 kwenye msimamo wa ligi.
Pia kamati ya tuzo imemchagua meneja wa uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga, Nassor Makau kuwa meneja bora wa uwanja wa mwezi kutokana na kufanya vizuri katika menejimenti ya matukio na masuala ya miundombinu uwanjani.