Feitoto kuufungua msimu wa 2026/27 Bukombe
Sisti Herman
August 25, 2026
Share :

Baada ya kukosekana kwa michezo mitatu akitumikia adhabu ya kadi nyekundu hatimaye kiungo mshambuliaji wa Azam FC, Feisal Salum ‘Feitoto’ anatarajiwa kurejea uwanjani Ijumaa katika mchezo wa timu yake dhidi ya Geita Gold.
Feisal aliikosa michezo mitatu ya kwanza ambayo ni ya timu za Polisi Tanzania, TRA United (Arusha) na Pamba Jiji ya Jijini Mwanza na alipewa kadi nyekundu msimu uliopita katika pambano la Fainali ya CRDB Federation Cup dhidi ya Simba iliyochezwa Pemba kwenye Uwanja wa Gombani.
Nyota huyo atarejea Ijumaa ya Agosti 28 katika mchezo huo wa Ligi Kuu Bara, utakaochezwa katika Uwanja wa Bukombe, Geita.





