Feitoto na Aziz Ki nani kuwa mfungaji bora leo?
Sisti Herman
May 28, 2024
Share :
Wakati ligi kuu Tanzania bara ikielekea ukingoni leo kwa mechi za mzunguko wa mwisho kuchezwa, vita kubwa inahusisha wanaowania tuzo ya mfungaji bora wa msimu ambayo mbio zake imebaki kwa wachezaji wawili, Stephanie Aziz Ki wa Yanga na Feisal Salum wa Azam.
Hizi hapa takwimu zao hadi sasa;
Feisal Salum
- Mechi - 29
- Dakika 2495
- Magoli - 18
- Asisti - 7
- Magoli ya penalti - 1
Aziz Ki
- Mechi - 26
- Dakika 2095
- Magoli - 18
- Asisti - 8
- Magoli ya penalti - 3
Mechi zao za leo;
Yanga vs Tanzania Prisons
Azam vs Geita Gold
Je unadhani nani ataibuka mfungaji bora leo?