Felix Tshisekedi amuita Kagame mvamizi na mhalifu
Eric Buyanza
April 29, 2024
Share :
Kwenye mahojiano maalumu na DW, Rais wa Kongo Felix Tshisekedi amesema kikwazo kwa amani katika kanda la Maziwa Makuu ni jirani yake rais wa Rwanda Paul Kagame.
Rais Tshisekedi anasema yuko tayari kwa mazungumzo na rais wa Rwanda Paul Kagame, huku akitupilia mbali uwezekano wa mazungumzo na kundi la waasi la M23.
''Nimekuwa nikisema kila mara kwamba siwezi kamwe kukutana na waasi wa M23, sababu ni moja pekee: Ni vibaraka ambao walitengenezwa kwa ajili ya kuhalalisha uvamizi dhidi ya nchi yangu ya Kongo. Lakini kiuhalisia, mvamizi halisi, mhalifu halisi, ni Paul Kagame. Na ninataka kukutana naye sio kwa lengo la kumsihi au kujadiliana naye chochote, bali kwa ajili ya kumwambia wazi, ana kwa ana, kwamba yeye ni mhalifu, na lazima asitishe.", alisisitiza Tshisekedi.
Tshisekedi amesema anazingatia pia miito iliyotolewa na nchi washirika wa Kongo kwa ajili ya kuweko na usitishwaji mapigano ili kuipa nafasi juhudi ya kutafuta amani.
DW