pmbet

Ferguson alikuwa na akili nyingi - Van Persie

Sisti Herman

April 9, 2024
Share :

Aliyekuwa mshambuliaji wa Manchester United, Arsenal na Uholanzi Robin Van Persie akimzungumzia kuhusu aliyekuwa kocha wa Manchester United Sir Alex Ferguson amesema alikuwa kocha wa tofauti sana na mwenye akili nyingi.

"Tulitoka nyuma mara 26 msimu huo. Nguvu ya akili ilikuwa isiyoaminika, Fergie alikufanya ujieleze kila wakati. Wakati fulani angeingia na kusema, 'Vijana, nitaanzia wapi? Inachosha! Hebu waza mimi, mwenye umri wa miaka 72, nikitazama mchezo wa aina hii?'

"Nifurahishe. Jaribu kupiga pasi zaidi ya mita 40. Jaribu kupiga chenga. Sijali kama itaenda vibaya. Ninataka mchangamke, jaribuni tafadhali ufanye mchezo kuwa mwepesi, tafadhali.'

"Alikuwa genius.”

Alimaliza hivyo RVP akimuelezea kocha huyo ambaye alimsajili kutoka Arsenal nakwenda kutwaa taji la EPL pamoja na kuwa mfungaji bora.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet