pmbet

Fetty ataja siri za Simba zilizowaua Yanga

Sisti Herman

January 4, 2024
Share :

Mchezaji mwandamizi wa Simba Queens Fatuma Issa “Fetty Densa” ametaja siri ya ushindi walioupata jana baada ya kuwafunga watani zao Yanga Princess kwenye mchezo wa raundi ya 3 ya ligi kuu wanawake Tanzania (TWPL) uliopigwa dimba la Azam Complex, Chamazi.

 

“Yanga walikuwa bora lakini hawakutupa mechi ngumu kama ile ya ngao ya jamii (iliyochezwa mwezi uliopita) kwasababu benchi la ufundi chini ya kocha Mgunda liliboresha mapungufu mengi ya mechi ile hasa ya kutumia vyuema nafasi tunazotengeneza tunamshukuru Mungu tukawa watulivu kufuata maelekezo ya waalimu tukapata matokeo” ameeleza Fetty kwenye mahojiano na PM Sports mara baada ya mchezo huo.

 

Kuhusu nani mchezaji bora wa mchezo kwa maoni yake, anaendelea Densa “Danella alikuwa kwenye kiwango bora sana, utulivu wakati wa kufanya maamuzi kwangu huyo ndio mchezaji bora wa mchezo japo wachezaji wote walikuwa kwenye kiwango bora na kujituma kupambania nembo ya Simba na hata morali ya wachezaji ipo juu mno” alimaliza Fetty ambaye pia ni mjasiriamali kupitia jina na chapa yake ya Densa Brand inayohusika na uuzaji na usambazaji wa mavazi na sabuni

 

Baada ya ushindi hupo Simba Queens sasa wamefikisha alama 9, baada ya kushinda michezo yote mitatu ya mwanzo ya ligi hiyo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet