pmbet

FIFA kuanzisha mpango wa amani Gaza

Eric Buyanza

February 21, 2026
Share :

FIFA imeanzisha mpango wa kuleta amani Mashariki ya Kati kupitia mradi wa 'Gaza United'.
Mpango huo unahusisha ujenzi wa miundombinu ya michezo, ikiwa ni pamoja na uwanja wa taifa wenye uwezo wa kubeba watu 20,000, viwanja vidogo 50, viwanja 5 vya mpira wa miguu, na chuo cha FIFA.

Mradi huu ni matokeo ya ushirikiano kati ya FIFA na Bodi ya Amani, iliyoanzishwa na Rais wa Marekani Donald Trump.
Lengo la mradi huu ni kuleta maendeleo na amani katika eneo la Gaza, ambalo limeathiriwa na vita kati ya Israel na Hamas. 

FIFA inatamani kuongeza dola milioni 75 kwa ajili ya mradi huu, ambao unatarajiwa kutengeneza fursa za ajira, kukuza ushiriki wa vijana kwenye michezo na kuimarisha uchumi wa ndani. 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet