pmbet

FIFA kuitoa Urusi kwenye kifungo

Sisti Herman

February 4, 2026
Share :

 

Rais wa FIFA Gianni Infantino ametangaza kuwa FIFA inafikiria kuiondolea Urusi kufungo cha kushiriki katika mashindano ya kimataifa.

“Lazima tulifikirie jambo hili bila shaka yoyote. kifungo hiki hakijafanikisha lolote; imeishia tu kuleta hali ya kukatishwa tamaa na chuki zaidi. Kuruhusu wavulana na wasichana kutoka Urusi kucheza mpira wa miguu katika sehemu nyingine za Ulaya kunaweza kusaidia,” alisema Rais huyo wa FIFA.

Urusi ilifungiwa kushiriki mashindano ya FIFA na UEFA tangu mwaka 2022 kufuatia uvamizi wake nchini Ukraine.

Kauli ya Infantino inaashiria mabadiliko makubwa katika siasa za michezo, akilenga kuwatenganisha wachezaji vijana na masuala ya kisiasa ya nchi yao.

Hatua hii inatarajiwa kuzua mijadala mikali, huku baadhi ya nchi zikiunga mkono na nyingine zikipinga kurejea kwa Urusi uwanjani wakati vita bado vinaendelea.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet