FIFA kumchunguza Eto'o
Sisti Herman
February 2, 2024
Share :
Kamati ya maadili ya Shirikisho la soka duniani (FIFA) limepokea tuhuma zinazomhusu Rais wa Chama cha soka cha Cameroon (Fecafoot), Samuel Eto’o za kuhusika na upangaji wa matokeo, kutoa vitisho, kusababisha vurugu na matumizi mabaya ya madaraka.
Makamu wa rais wa zamani wa Fecafoot, Henry Njalla Quan Junior amemtuhumu Eto'o na sasa tuhuma hizo zinafanyiwa uchunguzi na Fifa na Shirikisho hilo la soka la Afrika ambao awali iliwahi kushauriwa kumtoa staa huyo wa zamani wa Barcelona katika nafasi yake kutokana na mfululizo wa matukio tata.
Njalla Quan Junior amedai kwamba mechi kati ya akademi yake na Kumba City FC ilipangwa matokeo na Eto’o, akieleza tukio hilo kama moja ya “kashfa kubwa kabisa maishani”. Bosi huyo wa Cameroon pia anatuhumiwa kupanga matokeo ya timu ya “rafiki yake wa karibu“ Valentine Nkwain ipande daraja. Victoria United ikapanda daraja baada ya kushinda mechi 11 kati ya 17 za mwisho wa msimu licha ya kupoteza mechi nne kati ya saba za kwanza za msimu huo.