FIFA kuukagua uwanja wa Barcelona
Eric Buyanza
March 5, 2026
Share :

Ujumbe wa kiufundi kutoka FIFA utafika nchini Hispania na Ureno wiki ijayo kwa ajili ya ukaguzi wa kina wa viwanja vinavyotarajiwa kuwa wenyeji wa Kombe la Dunia la FIFA 2030.
Ujumbe huo utakagua viwanja kama vile Spotify Camp Nou huko Barcelona, Zaragoza, Madrid, Las Palmas, Sevilla, A Coruna, Bilbao, na San Sebastian.
Ujumbe huu ni hatua muhimu katika mchakato wa kuandaa Kombe la Dunia la 2030, ambalo litafanyika nchini Hispania, Ureno, na Morocco.
Mnamo Desemba 2024 FIFA ilithibisha Mataifa hayo matatu kuwa wenyeji.
Ukaguzi huo utakazia miundombinu, maendeleo ya ujenzi, vifaa, masuala ya kisheria, na kifedha ya viwanja hivyo kabla ya kuthibitisha viwanja rasmi mnamo Desemba 2026.
Na, kulingana na ripoti, moja ya vituo muhimu itakuwa Barcelona, ambapo wakaguzi watachunguza maendeleo ya Spotify Camp Nou ambao unafanyiwa ukarabati.
Spotify Camp Nou utaongezeka uwezo wa kuingiza mashabiki 105000 maboresho yakikamilika na utakuwa uwanja mkubwa kuliko vyote barani Ulaya.





