pmbet

FIFA na FA wafunguka kuhusu kadi ya Bluu

Sisti Herman

February 9, 2024
Share :

Wakati Bodi ya Vyama vya Kimataifa vya Mpira wa Miguu (IFAB) inayohusika na sheria za mchezo wa mpira wa miguu likiwa katika mazungumzo na waamuzi ili kuleta sheria mpya ya matumizi ya kadi ya bluu itakayotumika kwa makosa ya kuonyesha ishara ya kupinga uamuzi wa mwamuzi husika atakayekuwa anasimamia mchezo, Shirikisho la Soka Duniani (Fifa) limetoa ufafanuzi kuwa bado mpando huo haujaauliwa kama taarifa za mitandao ya kijamii mbalimbali zinavyoeleza.

 

"FIFA inapenda kufafanua kwamba ripoti za kile kinachoitwa 'kadi ya bluu' katika viwango vya juu vya soka si sahihi na ni za mapema na Majaribio yoyote kama hayo, ikiwa yatatekelezwa, yanapaswa kuwa ya majaribio kwa njia ya uwajibikaji katika viwango vya chini, msimamo ambao FIFA inakusudia kusisitiza wakati kipengele hiki cha ajenda kinajadiliwa katika AGM ya IFAB mnamo 1 Machi."

Lengo kubwa la kadi hiyo inayotarajiwa kuzinduliwa kesho Ijumaa ni kwamba itatolewa kwa mchezaji atakayefanya madhambi kwa mwenzake, kupingana na uamuzi wa mwamuzi wa kati, mshika kibendera 'linesman' au kamisaa 'fourth official'.

Ikiwa mchezaji atapata kadi hiyo atatoka nje ya uwanja kwa dakika 10 huku mchezo unaendelea na huu ni utambulisho wa kwanza tangu kadi ya njano na nyekundu zilivyoanza kutumika 1970.

Endapo mchezaji atapata kadi hiyo kwa mara ya pili, atatolewa nje moja kwa moja kama inavyokuwa akipata kadi mbili za njano.

Majaribio hayo tayari yalishaanza kutumika katika ligi ndogo huko Wales, lakini yalisitishwa kutokana na kutopitishwa mamlaka za juu soka.

Licha ya sheria hiyo kusubiriwa kuanza kutumika, lakini vyombo vya habari kutoka England vimeweka wazi kwamba Chama cha Soka nchini humo (FA) hakina lengo la kuanza kutumia katika michezo ya Ligi Kuu England (EPL), Kombe la Ligi (EFL) na lile la FA.

Ofisa MTendaji Mkuu wa EPL, Tony Scholes amesema licha ya majadilino na Bodi ya Vyama vya Kimataifa vya Mpira wa Miguu (IFAB) inayohusika na sheria za mchezo huo, lakini hawana lengo la kuitumia kwa sasa.

"Sifikirii kama tunaweza kutumia katika michuano yetu mikubwa. Hiyo ni kama tunataka kuzitumia au laah!, ila hatutatumia msimu ujao," amesema Scholes.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet