pmbet

FIFA Rankings; Tanzania ilivyopanda nafasi 10 ndani ya Miezi 10

Sisti Herman

October 9, 2024
Share :

Wakati tukishuhudia maendeleo ya kasi vilabu vya Tanzania kwenye michuano ya kimataifa sambamba na ukuaji wa ligi kuu Tanzania bara, Tanzania pia imetajwa kuwa moja ya nchi zinazokuwa kwa kasi sana kwenye viwango vya ubora duniani vinavyotolewa na Shirikisho la soka duniani (FIFA) baada ya kukua kwa kasi hadi kufikia nafasi ya 110, ikipanda nafasi zaidi ya 10 ndani ya miezi 10 tu.



Katika kipindi cha miezi 10 iliyopita Tanzania imepanda nafasi hizo zaidi ya 10 baada ya mwendelezo wa matokeo mazuri ya kikosi cha timu ya Taifa Tanzania kwenye michuano mbalimbali, huku ikipata matokeo haya;

 

- Idadi ya mechi ilizocheza 10

- Idadi ya mechi ilizoshinda 3

-Idadi ya mechi ilizopoteza 3

-Idadi ya mechi zilizomalizika kwa sare 4


Kwenye viwango vya FIFA vilivyotolewa mwezi Disemba mwaka 2023, Tanzania ilikuwa nafasi ya 121, kisha ikapanda nafasi 2 kwenye viwango vilivyochapshwa mwezi Februari hadi kufika nafasi ya 119 ikikusanya alama 1161.

 


 

 

 


Kwenye viwango vya FIFA vya mwezi June 2024, Tanzania ilipanda nafasi 5 kutoka nafasi ya 119 kwenye viwangio vya mwezi Februari na Aprili hadi ya 114 huku ikifikisha alama 1175.

 

 

 



Kwenye viwango vya FIFA vya mwezi Julai 2024, Tanzania ilipanda kwa nafasi 1 kutoka nafasi ya 114 kwenye viwango vya awali hadi nafasi ya 113 duniani.
 

 


Kwenye viwangi vya FIFA vya mwisho kuchapishwa Septemba 19 2024, Tanzania imepanda nafasi 3 zaidi kutoka nafasi ya 113 mwezi Julai hadi nafasi ya 110 duniani huku ikifikisha alama 1188.

 


Kwa mwendelezo huo bora, Tanzania inatajwa kuwa moja kati ya timu ambazo zinaendelea kukua kwa kasi kwenye viwango vya FIFA.

 

Kesho timu ya Taifa ya Tanzania ina mchezo wa 4 wa hatua ya makundi ya kuwania kufuzu kombe la Mataifa ya Afrika kwa kundi H dhidi ya timu ya Taifa ya Congo DR, ugenini kisha kucheza nao tena siku 5 baadae nyumbani.

 

Kila la Kheri Tanzania.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet