FIFA yachunguza tuhuma za ubaguzi wa rangi dhidi ya ishowspeed
Eric Buyanza
July 8, 2026
Share :

Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA) limeanzisha uchunguzi kufuatia madai ya vitendo vya ubaguzi wa rangi vilivyomlenga mwanamitandao maarufu IShowSpeed alipokuwa akihudhuria mechi ya Kombe la Dunia.
IShowSpeed, anayefahamika zaidi kwa jina la Speed, ni mmoja wa watayarishaji wa maudhui wanaofuatiliwa zaidi duniani, akiwa na zaidi ya wafuasi milioni 57 kwenye mtandao wa YouTube.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, FIFA inachunguza tukio hilo ili kubaini kilichotokea na kuchukua hatua stahiki iwapo madai hayo yatathibitishwa.
Shirikisho hilo limesisitiza kuwa halitavumilia aina yoyote ya ubaguzi wa rangi au vitendo vya chuki katika mashindano yake, likiahidi kushirikiana na mamlaka husika kuhakikisha mazingira salama na yenye heshima kwa mashabiki na wageni wote wanaohudhuria mechi za Kombe la Dunia.
Hadi sasa, FIFA haijatoa taarifa kuhusu watu wanaodaiwa kuhusika na tukio hilo wala hatua za kinidhamu zinazoweza kuchukuliwa wakati uchunguzi ukiendelea.





