pmbet

FIFA yasimamisha shughuli za soka nchini Nepal

Eric Buyanza

June 25, 2026
Share :

Shirikisho la mpira wa miguu dunia FIFA limekisimamisha Chama cha Soka cha Nepal (ANFA) mara moja, hadi itakapotangazwa tena, na kusababisha pigo kubwa kwa mpira wa miguu nchini humo.

 

"Tunawaarifu kwamba, kutokana na uamuzi uliochukuliwa na Ofisi ya Baraza mnamo tarehe 24 Juni 2026, ANFA imesimamishwa hadi itakapotangazwa tena kwa mujibu wa Kifungu cha 16 cha Sheria za FIFA," taarifa hiyo ilisomeka.

 

Kutokana na kusimamishwa huko, timu za taifa na vilabu vya vya Nepal vitazuiwa kushiriki katika mashindano ya kimataifa yaliyoidhinishwa na FIFA na Shirikisho la Soka la Asia (AFC).

 

Kusimamishwa huko pia kunasitisha utoaji wa programu za maendeleo za FIFA na AFC, mipango ya mafunzo, na kozi za elimu kwa ANFA, wanachama wake, na maafisa wake.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet