pmbet

FIFPRO yaijia juu Bayern kisa Musiala

Sisti Herman

November 22, 2026
Share :

 

Shirikisho la Wachezaji wa Kulipwa Duniani (FIFPRO) limeikosoa vikali Bayern Munich kufuatia kauli za baadhi ya viongozi wa klabu hiyo kuhusu mustakabali wa mkataba wa nyota wao, Jamal Musiala, ambaye anaendelea kuuguza majeraha.

Kwa mujibu wa FIFPRO, kauli hizo zinaweza kuwa njia ya kumwekea Musiala shinikizo katika masuala ya kimkataba, huku likisisitiza kuwa majeraha au kushuka kwa kiwango cha mchezaji havipaswi kutumika kama sababu ya kushinikiza mabadiliko ya makubaliano yaliyopo.

Aidha, FIFPRO imeitaka Bayern kuheshimu haki za Musiala na kujadili masuala ya mkataba wake kwa faragha, ikionya kuwa mijadala ya hadharani inaweza kuathiri afya ya akili ya mchezaji huyo.

Hata hivyo, Mtendaji Mkuu wa Bayern Munich, Jan-Christian Dreesen, amekanusha madai ya kumwekea Musiala shinikizo, akisisitiza kuwa nyota huyo anahitaji muda wa kurejea katika kiwango chake bora.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet