Filamu ya Micheal Jackon yavunja rekodi ya mauzo Dunia nzima.
Joyce Shedrack
May 18, 2026
Share :
Filamu ya wasifu wa mfalme wa pop duniani, Michael Jackson yenye jina la Michael, inaendelea kufanya vizuri kwenye mauzo ya box office duniani tangu ilipoachiwa rasmi April 24, 2026.
Mpaka sasa filamu hiyo imeingiza zaidi ya dola milioni 700 sawa na zaidi ya Tsh trilioni 1.8 duniani kote, na kuendelea kushika nafasi ya kwanza kwenye box office kwa wiki nyingine mfululizo.
Filamu hiyo imefanikiwa kuzipita filamu nyingine kubwa kama The Devil Wears Prada 2 pamoja na Obsession, ambazo pia zinafanya vizuri kwenye sinema mbalimbali duniani.
Michael inamuonyesha Michael Jackson kuanzia maisha yake akiwa kwenye kundi la Jackson 5 hadi kuwa mmoja wa wasanii wakubwa zaidi duniani. Filamu hiyo imeongozwa na Antoine Fuqua huku Jaafar Jackson, ambaye ni mpwa wa Michael Jackson, akiigiza nafasi ya Michael.





