Finland yatajwa nchi yenye furaha zaidi duniani, Tanzania ya 136
Eric Buyanza
March 21, 2025
Share :
Ripoti ya Dunia ya Furaha ya mwaka 2025, iliyotolewa Machi 20, imeitangaza Finland kuwa nchi yenye furaha zaidi duniani kwa mwaka wa 8 mfululizo.
Nchi zinazofuatia ni Denmark (2), Iceland (3), Sweden (4) huku Uholanzi ikishika nafasi ya 5.
Tanzania imechukua nafasi ya 136 kati ya mataifa 147 katika ripoti hiyo iliyotangazwa jana wakati dunia ilipokuwa ikiadhimisha Siku ya Kimataifa ya Furaha.
Kwenye orodha hiyo kwa upande wa nchi zenye furaha zaidi Afrika, Mauritius imeshika nafasi ya kwanza, ikifuatiwa na Libya iliyokamata nafasi ya pili huku Tanzania ikikamata nafasi ya 32.
Kwa Libya kukamata nafasi ya pili kama nchi yenye furaha zaidi Afrika kumewashangaza wengi kutokana na machafuko na vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyoendelea nchini humo.