Fisi aua mmoja, mwanafunzi chuo kikuu ajeruhiwa
Eric Buyanza
February 8, 2024
Share :
Mtu mmoja amefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa vibaya baada ya kushambuliwa na kundi la fisi karibu na Chuo kimoja kikuu nje kidogo ya jiji la Nairobi.
Mmoja wa waliojeruhiwa ni mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Multimedia aliyeshambuliwa katika barabara moja inayopakana na Mbuga ya Taifa ya Wanyama ya Nairobi huko Ongata Rongai.
Kisa hicho kimepelekea wanafunzi kutoka chuo hicho kuandamana wakilalamikia usalama wao. Polisi walitumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya wanafunzi hao.
Shirika la Wanyama Pori nchini Kenya (KWS) linasema kikosi kilichotumwa kuchunguza kisa hicho kilipata sehemu za mwili wa mtu katika eneo la tukio.