pmbet

Fisi aua watoto 3 wa familia moja

Eric Buyanza

April 9, 2024
Share :

Watoto watatu wa familia moja, wakazi wa kitongoji cha Gengeni Kata ya Kambikatoto Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya, wamefariki dunia baada ya kuvamiwa na kuliwa na fisi wakiwa ndani ya nyumba yao, huku wazazi wao wakiwa wamejeruhiwa vibaya. 

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Abdi Issango, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo wakati akizungumza na waandishi, ambapo ameeleza kuwa nyumba waliyokuwa wamelala watoto hao haikuwa na mlango na ipo jirani na pori la hifadhi ya Rungwa. 

Amewataja watoto waliofariki kuwa ni Samweli Shigela (5), Kasunzu Shigela (3) na Ngasa Shigela mwenye umri wa mwaka mmoja. Amesema baada ya tukio hilo, pia fisi huyo aliwaua kondoo wawili na kisha akakimbilia katika Hifadhi ya Rungwa iliyopo katika Kambikatoto. 

Amesema majeruhi wamelazwa katika Hospitali ya Mtakatifu Gasper – Itigi, Wilaya ya Manyoni, Mkoa wa Singida kwa matibabu zaidi. Wakati huohuo, kutokana na tukio hilo askari wa Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na askari wa wanyama pori kutoka pori la akiba la Rungwa na wananchi wa Gengeni wamefanya msako na kufanikiwa kumuua fisi huyo. Hata hivyo, kamanda huyo amewataka wananchi kuchukua tahadhari kwa kufunga milango, ili kujikinga na majanga ya kuvamiwa na wanyama.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet