pmbet

FKF kukata mzizi wa fitna sakala ya Sharks na Mombasa United

Sisti Herman

October 8, 2026
Share :

 

Kufuatia kusimamishwa kwa mechi ya mchujo ya kupanda au kushuka daraja kati ya Kariobangi Sharks na Mombasa United siku ya Jumanne, Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) limeanza mchakato wa kuamua hatua zinazofuata.

Wadau wote husika wamewasilisha ripoti zao kwa FKF, huku klabu zote mbili zikielekezwa kuwasilisha maelezo yao kwa maandishi kabla ya siku ya Alhamisi.

Timu hizo mbili pia zinatarajiwa kufika mbele ya Kamati ya Ligi na Mashindano ya FKF (LCC) siku ya Ijumaa asubuhi, ambapo zitapata fursa ya kutoa maelezo yao kuhusu tukio hilo.

FKF inasema imedhamiria kuhitimisha suala hilo haraka iwezekanavyo na imechukua hatua zinazohitajika ili kuhakikisha mchakato huo unaharakishwa.

Wakati huo huo, maafisa wa usalama wa FKF, maafisa wa mechi na wahudumu wa uwanjani wametoa maelezo yao katika Kituo cha Polisi cha Lang’ata huku uchunguzi kuhusu matukio yaliyosababisha kusimamishwa kwa mechi hiyo ukiendelea.

Mechi hiyo, ambayo ilikuwa ni mchezo wa marudiano wa mchujo wa kupanda au kushuka daraja, ilisitishwa kabla ya muda wake wa kawaida kufuatia vurugu zilizotokea, na hivyo kuacha matokeo ya mchuano huo yakiwa bado hayajajulikana.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet