Florent Ibenge kutimkia Timu ya Taifa ya Mali.
Joyce Shedrack
May 27, 2026
Share :
Taarifa kutoka Nchini Mali zinaripoti kuwa Shirikisho la soka nchini Mali limteua Kochawa Azam FC raia wa DR Congo, Florent Ibenge, kuwa Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Mali akichukua nafasi ya kocha Mbelgiji Tom Saintfiet aliyejiuzulu siku chache zilizopita.
Ibenge amechaguliwa kati ya Makocha watano walioingia hatua ya mwisho ya mchakato wa kutafuta Kocha Mkuu wa Taifa hilo akiwapiga chini Mohamed Magassouba, Badou Zaki, António Conceição na Anthony Da Silva.
Bado hakuna taarifa rasmi kutoka kwenye shirikisho la Mali wala kwa Azam Fc kuhusu kocha huyo ambaye alijiunga na klabu hiyo ya Chamazi Julai 5 2025 akitokea Al Hilal ya Sudan.





