pmbet

Foden apeleka kiama United kwenye Derby ya Manchester

Sisti Herman

March 3, 2024
Share :

Klabu ya Manchester City imeshinda mchezo wa ligi kuu Uingereza kwa kuwapiga kipigo cha mbwa mwizi watani zao wa jiji moja Manchester United goli 3-1.

Man Utd walianza kufunga kwa bao la Marcus Rashford lililodumu kwa kipindi chote cha kwanza kabla ya kipindi cha pili upepo kuwageukia na kuchabangwa mabao matatu yaliyofungwa na Phil Foden aliyefunga mawili huku mshambuliaji mwenye njaa kali Erling Halland akitupia msumari wa mwisho.

Kufikia hapo Man City inaendeleza ushindani kwa Liverpool kwenye mbio za ubingwa huku United ikipoteza matumaini taratibu kwenye mbio za kuwania nafasi za kucheza michuano ya Ulaya msimu ujao baada ya kuendelea kujisimika nafasi ya 6 kwenye msimamo wa ligi.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet