"Foden atashinda Ballon D'or" Tom Frank
Sisti Herman
February 20, 2024
Share :
Kocha wa Brentford Thomas Frank alipokuwa akizungumza na kituo cha habari cha Sky Sports amemtaja kiungo mshambuliaji wa anchester City na timu ya Taifa ya Uingereza Phil Foden kuwa ndiye mchezaji wa Uingereza ambaye anaweza kushinda tuzo ya Ballon d’Or kwa miaka ya karibuni.
Maoni hayo ya Frank yanaenda sambamba na yale ya beki wa zamani wa Uingereza na Manchester United Rio Ferdinand ambaye aliweka wazi kuwa Foden ni zaidi ya Bukayo Saka.