Foden Mchezaji bora wa msimu EPL
Joyce Shedrack
May 18, 2024
Share :
Mchezaji wa klabu ya Manchester City Phil Foden ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu Uingereza msimu wa 2023/24.
Foden ambaye msimu huu amekuwa na kiwango bora hadi sasa amecheza mechi 34 na kufunga magoli 17 na asisti 8 akiwazidi Erling Halland wa Man City, Alexander Isak wa Newcastle, Martin Odegaard wa Arsenal, Cole Palmer wa Chelsea, Declan Rice wa Arsenal na Ole Watkins wa Aston Villa.