"Foden ni mchezaji bora duniani kwasasa" - Pep
Sisti Herman
March 4, 2024
Share :
Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amebainisha wazi kuwa kiungo mshambuliaji wa klabu hiyo na timu ya Taifa ya Uingereza Phil Foden kwasasa ndiye mchezaji bora zaidi duniani.
"Ni mchezaji bora kwenye ligi kuu Uingereza kwasasa na pengine duniani kote, ngumu kuamini, lakini ipo hivyo kwasasa" alisema Pep baada ya mchezo dhidi ya Man Utd.
Kwenye mchezo dhidi ya watani zao Manchester United kiungo huyo mshambuliaji alitupia mabao mawili kambani wakishinda 3-1.