Fofana wa Chelsea alalamika kuitwa 'nyani' instagram
Sisti Herman
February 22, 2026
Share :

Beki wa Chelsea, Wesley Fofana, ameanika mfululizo wa jumbe za matusi alizopokea kupitia 'Direct Message' (DM) kwenye mtandao wa Instagram kufuatia kadi nyekundu aliyopata dhidi ya Burnley.
Fofana alitumia ukurasa wake wa 'Story' kuonyesha picha za skrini (screenshots) za jumbe za chuki zilizoelekezwa kwake, jambo ambalo limezua tena mjadala kuhusu unyanyasaji wa mitandaoni wanaopitia wachezaji baada ya matokeo mabaya uwanjani.





