Fountain Gater Princess kuweka Kambi Dar
Sisti Herman
April 9, 2024
Share :
Klabu ya Fountain Gate Princess kupitia idara yao ya habari imethibitisha kuwa wachezaji kambini kujiandaa na ngwe ya pili ya ligi kuu wanawake (WPL).
"Timu imerejea kwanye Uwanja wake wa mazoezi leo Asubuhi, ikiwa ni maandalizi ya kuelekea kwenye duru ya pili ya Ligi Kuu Wanawake Tanzania Bara.
"Timu inatarajia kuanza safari wiki hii kutoka Dodoma na kuweka Kambi fupi Dar es salaam, kabla ya kuanza safari pia kuelekea kwenye mji wa Kihistoria wa Lindi.
"Ikiwa Lindi, Fountain Gate Princess itacheza mechi ya kwanza kwenye mzunguko wa pili na Amani Queens, mchezo unaotarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Ilulu, mkoani Lindi".
Fountain wapo nafasi ya 5 kwenye msimamo wa ligi hiyo inayoongozwa na Simba Queens.