pmbet

Fountain kuiwakilisha Tanzania kesho Misri mashindano ya vijana

Sisti Herman

May 2, 2024
Share :

Timu ya Vijana ya Fountain Gate ya Vijana wenye umri chini ya miaka 19 itashuka dimbani kesho katika machuano maalum ya SPOCS U19 SCOUTING CUP 2024 ambayo hufanyika kwa siku 10 ikihusisha mataifa 12 yaliyoandaliwa na wasaka vipaji wa Spocs Consulting yakiwa na lengo la kutafuta vijana kutokea Afrika ambapo watakaofanya vizuri watapata fursa ya kwenda kucheza soka barani Ulaya.

Fountain watacheza kesho dhidi ya klabu ya ENPPI, kisha watashuka dimbani siku mbili baadaye dhidi ya ZED FC kisha kumaliza dhidi ya Egypt u17 siku ya tarehe 7.

Rais wa Singida Fountain Gate,Japhet Makau amesema mashindano hayo ni jukwaa kwa Vijana wa kitanzania kuonyesha uwezo wao utakaowafungulia milango ya kuendeleza vipaji vyao katika bara la Ulaya.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet