pmbet

Fountain wafunguka kocha kuondoka

Sisti Herman

December 31, 2023
Share :

Aliyekuwa kocha wa viungo wa Simba Queens, kocha wa viungo wa Fountain Gate Princess na timu ya Taifa ya wanawake ya Zimbabwe Brenda Chaoor kupitia mitandao yake ya kijamii ameaga kuendelea kuitumikia Fountain Gate Princess baada ya mkataba wake kutamatika.

 

Kupitia PM Sports  mratibu wa Fountain Gate Princess Issa Liponda “Issa Mbuzi” amethibitisha kuwa ni kweli mkataba wa kocha huyo raia wa Zimbabwe umeisha kuendelea kuitumikia klabu hivyo uongozi umebariki yeye kutafuta changamoto kwingine.

 

“Ningependa kuwajulisha mashabiki, marafiki zangu na wale wanaonipenda na sanaa yangu kwamba mkataba wangu na Klabu ya Soka ya Fountain Gate umefikia mwisho wake.Uamuzi kutoka kwa wakala wangu wa michezo na mimi ulifanyika miezi 2 kabla ya tarehe ya kumalizika kwa mkataba wa kutoongeza muda wangu wa kukaa katika Klabu hio kwa kuwa ni wakati wa kuingia katika changamoto mpya na ukuaji wa kibinafsi. Imekuwa furaha kutumikia huko na ninathamini kila dakika niliyokuwa nayo na wachezaji, timu ya ufundi na mashabiki ilikuwa ya thamani kubwa, ningependa kutaja shukrani za pekee kwa Bwana Makau (Japhet, Mkurugenzi wa taasisi) kwa fursa ninayoithamini sana. naitakia Timu, Mwekezaji, Wachezaji, Timu ya Ufundi na Mashabiki kila la kheri katika harakati zao za kutafuta utukufu”. inaeleza taarifa ya kuaga ya kocha huyo kupitia mtandao wake wa kijamii wa instagram.
 

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet