pmbet

Frank Lampard airejesha Covenrty City ligi kuu baada ya miaka 25.

Joyce Shedrack

April 18, 2026
Share :

Klabu ya Coventry City imerejea kwenye Ligi Kuu ya Uingereza kwa mara ya kwanza baada ya miaka 25 kufuatia kujikatia tiketi ya kupanda daraja kutoka Championship kutokana na sare ya 1-1 waliyoipata dhidi ya Blackburn Rovers usikuwa kuamkia leo.

 

Klabu hiyo ilishiriki Ligi Kuu kwa mara ya kwanza msimu wa 1992-93 na hawajawahi kurejea tangu waliposhuka daraja msimu wa 2000-01 itashiriki ligi kuu msimu ujao baada ya msimu mzuri sana katika daraja la pili chini ya kocha Frank Lampard.

Nach 25 Jahren: Coventry City kehrt in die Premier League zurück

Coventry walitumia miaka 34 mfululizo kwenye ligi ya juu ya Uingereza na walijulikana kwa kunusurika  mara nyingi kushuka daraja kabla ya hatimaye kushuka mwaka 2001. 

 

Kipindi kigumu zaidi cha Coventry kilikuwa waliposhuka hadi daraja la nne mwaka 2017, lakini wamepambana kurejea juu, na baada ya kupoteza fainali ya mchujo dhidi ya Luton Town mwaka 2023, wamefanya vizuri sana msimu huu wa Championship chini ya Lampard na kuhakikisha kurejea kwao kwenye Ligi Kuu wakiwa na mechi tatu mkononi.

 

 

 

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet