Fred ataja utofauti wa Ole Gunnar na Ten Hag pale Man United
Sisti Herman
October 5, 2026
Share :

Aliyekuwa kiungo wa Manchester United na Brazil, Fred amezungumzia utofauti wa waliokuwa makocha wa Mnachester United Ole Gunnar Solskjær na Erik Ten Hag:
“Kuna makocha ambao ni wazuri sana kimbinu lakini ni wabaya katika kulishughulikia kundi la wachezaji, na kuna wengine ambao ni wazuri sana katika kulishughulikia kundi lakini kimbinu ni ovyo kabisa.
“Kwa mfano, Solskjær alikuwa mzuri sana katika kulishughulikia kundi, lakini kimbinu aliwategemea Carrick na McKenna kama wasaidizi wake—kiasi kwamba baadaye walikwenda kufundisha ligi ya Championship na kupandisha timu zao daraja, hivyo walisaidia sana... yeye alijikita zaidi katika kuliunganisha kundi.
“Ten Hag alikuwa mtu mzuri sana na mwenye akili kimbinu, lakini katika kulishughulikia kundi alikuwa ovyo. Hakuweza kulimudu kabisa. Alikuwa akigombana na kila mtu.”
Chanzo: CharlaPodcast





