Frida Amani aweka rekodi ya kufanya show mbele ya Marais 150.
Joyce Shedrack
December 13, 2025
Share :
Msanii wa muziki Nchini na mtangazaji wa Clouds FM Frida Amani ameweka rekodi ya kutumbuiza mbele ya Marais na viongozi 150 kwenye mkutano wa "UNEA 7" unaowakutanisha viongozi wa nchi mbalimbali kujadili namna ya kutunza mazingira.
Staa huyo wa muziki wa hiphop anakuwa msanii wa kwanza duniani kutumbuiza kwenye jukwaa hilo na kuwakilisha utamaduni wa HipHop.
Frida Amani Mwaka Jana alitumbuiza mbele ya Marais 15 na mapema mwaka huu alifanya tena show mbele ya Rais Finland na hivi sasa amefanya tena mbele ya viongozi 150.





