Fukuza fukuza yaanza Ligi kuu, TRU United wamnyoa Ndayiragije
Eric Buyanza
September 8, 2026
Share :

Baada ya kuwa na mwendelezo wa kukosa matokeo ya ushindi tangu Ligi Kuu Bara ianze msimu huu, kikosi cha TRA United kimempa Thank You kocha wake Etienne Ndayiragije.
TRA United inapenda kuujulisha umma, wanachama, mashabiki na wadau wake wote kuwa timu yao imeachana na kocha huyo raia wa Burundi.
Kikosi hicho kimefikia makubaliano ya pande mbili ya kusitisha mkataba wa ajıra kati yao na kocha huyo, kuanzia leo tarehe 7 Septemba, 2026.
Uongozi wa TRA United unachukua fursa hil kumshukuru kwa dhati Kocha Ndayiragije kwa mchango wake mkubwa, weledi na huduma ya kipekee aliyoitoa kwa timu katika kipindi chote alichokuwa sehemu ya klabu.
Tunampongeza na kumtakia kila la kheri na mafanikio mema katika hatua inayofuata ya maisha na taaluma yake ya ukocha na Klabu itaendelea kuwasiliana na wanachama, mashabiki na wadau wake kuhusu hatua zaidi zinazohusiana na uongozi wa benchi la ufundi la timu.
Kocha huyo anakuwa kocha wa kwanza kupewa Thank You tangu kuanza kwa Msimu huu wa 2026/2027.





