Fundi wa mpira Haruna Niyonzima arejea nyumbani.
Joyce Shedrack
July 17, 2024
Share :
Kiungo wa zamani wa klabu ya Simba na Yanga Haruna Niyonzima amerejea nyumbani kwao Rwanda kuitumikia klabu yake ya zamani ya Rayon Sport.
Niyonzima mwenye umri wa miaka 34 amerejea Rayon aliyowahi kuitumikia mwaka 2006 na 2007 akitokea nchini Libya alikokuwa anaitumikia Al Ta'awon iliyomaliza nafasi ya tatu kwenye ligi ya nchini humo msimu uliopita.
Kiungo huyo fundi aliwahi kuvitumikia vilabu vitatu tofauti tofauti nchini humo kama Etincelles, APR, AS Kigali na Rayon Sport.