FUNDI YAMAL: Afikisha mchango wa mabao 20 ndani ya mechi 13
Eric Buyanza
October 12, 2026
Share :

Kinda hatari wa soka duniani, Lamine Yamal, ameendelea kuishangaza dunia baada ya kuweka rekodi ya kufikisha mchango wa mabao 20 (mabao 12 na pasi za mabao 8) ndani ya michezo 13 pekee ya msimu huu wa 2026/27, akiwa na klabu yake ya FC Barcelona pamoja na timu ya taifa ya Uhispania.
Kasi hii ya kutisha inamaanisha amefikia idadi hiyo ya mabao sita mapema zaidi ukilinganisha na msimu uliopita, ambapo ilimchukua jumla ya michezo 19 kufikisha idadi hiyo hiyo ya mchango wa mabao.
Wachambuzi wengi wa soka wamedai kuwa ikiwa ataendelea na kasi hii, anaweza kumaliza msimu akiwa na mchango wa mabao zaidi ya 45 hadi 50, jambo litakalomweka mstari wa mbele kuwania tuzo ya Ballon d'Or ya mwaka 2027.






