G7 wako tayari kuichukilia hatua Iran kwa kuiyumbisha kanda
Eric Buyanza
April 15, 2024
Share :
Viongozi wa nchi saba tajiri duniani (G7) wameonyesha kuiunga mkono Israel kufuatia shambulizi la Iran, na kusema wako tayari kuchukua hatua zaidi katika kujibu walichoita mipango ya kuiyumbisha kanda.
Katika taarifa kufuatia mkutano wa video, viongozi hao wa G7 walisema wanalaani vikali shambulio la Iran dhidi ya Israel.
Rais wa Halmashauri Kuu ya Ulaya Ursula von der Leyen amesema katika taarifa kuwa watatafakari vikwazo zaidi dhidi ya Iran kwa ushirikiano wa karibu na washirika wao, na hasa kuhusu mipango ya nchi hiyo ya droni na makombora.
Iran ilifanya shambulizi, lake la kwanza la moja kwa moja kwenye ardhi ya Israel, katika kulipiza shambulizi kali la angani lililodaiwa kufanywa na Israel na kuharibu jengo la ubalozi wake mdogo katika mji mkuu wa Syria Damascus mapema mwezi huu.
Shambulizi hilo lilijiri wakati vita kati ya Israel ha Hamas vikiendelea huko Gaza.