pmbet

Gabriel Jesus ajiunga na Barcelona

Sisti Herman

September 1, 2026
Share :

 

Klabu ya Barcelona imethibitisha rasmi kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil, Gabriel Jesus, akitokea katika klabu ya Arsenal ya nchini Uingereza.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka mtandao wa Sky Sports News, miamba hiyo ya ligi kuu nchini Uspania (LaLiga) imekubali kulipa ada ya usajili inayokadiriwa kufikia paundi milioni 8.6 ili kunasa saini ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 29.

Hatua hii inahitimisha kipindi cha Jesus klabuni Arsenal na kumfungulia ukurasa mpya katika soka la Uspania, ambapo Barcelona inatarajia uzoefu wake na uwezo wake wa kufumania nyavu utaongeza nguvu mpya kwenye safu yao ya ushambuliaji.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet