Gadiel avutwa Sauzi na kocha aliyemchezesha mido
Sisti Herman
January 26, 2024
Share :
Nyota wa zamani wa Azam FC, Yanga SC na Simba SC, Gadiel Michael Kamagi ametambulishwa kama mchezaji mpya wa klabu ya Cape Town Spurs ya Afrika Kusini akitokea Singida Fontaine Gate FC.
Gadiel anajiunga na Spurs ambayo inafundishwa na kocha Ernest Middendorp ambaye aliwahi kumfundisha akiwa Singida FGFC ambaye anakumbukukwa zaidi kwa tukio la kumpanga beki huyo wa pembeni kama kiungo wa kati kwenye mchezo wa kombe la shirikisho Afrika dhidi ya Future ya Misri huku akiwaacha viungo kama Morice Chuku na Yusuph Kagoma benchi.
Uamuzi uamuzi huo uliwashangaza viongozi wa juu wa Singida hadi kufikia hatua ya kumhoji kocha huyo raia wa Ujerumani na Afrika kusini hali iliyomfanya kocha huyo kufikia umauzi wa kujiuzulu baada ya mchezo mmoja kwa kile alichodai kuingiliwa kwenye majukumu yake na uongozi.
Taarifa rasmi ya Cape Town Spurs almaarufu ‘Urban Warriors’ yenye maskani yake Cape Town, Afrika Kusini imesema “Hakuna Matata na salamu kutoka Tanzania! Mchezaji wa Kimataifa wa Tanzania Gadiel Kamagi ni ‘Urban Warrior’”