Gadiel Kutimkia Sauzi
Sisti Herman
January 17, 2024
Share :
Rais wa klabu ya Singida Fountain Gate, Japhet Makau amethibitisha kuwa nahodha wao Gadiel Michael amejiunga na Cape Town Spurs ya ligi kuu nchini Afrika Kusini kwa mkataba wa mwaka 1.
Rais wa klabu ya hiyo Japhet Makau amethibitisha hilo leo hii ambapo amesema wanaendelea kufanya biashara ili kupunguza matumizi.
Mchana wa leo Gadiel ataanza safari ya kuelekea South Africa kwaajili ya kujiunga na timu yake mpya.