Gadner kuzikwa Jumanne Rombo
Sisti Herman
April 21, 2024
Share :
Mwili wa aliyekuwa mtangazaji wa kituo cha redio cha Clouds FM, Gardner Habash utaagwa kesho jijini Dar es Salaam na kuzikwa Jumanne Aprili 23, 2024 mkoani Kilimanjaro.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Kampuni ya Clouds Media Group, mwili huo atazikwa kijijini kwao Kikelelwa, kata ya Tarakea, wilayani Rombo, mkoani Kilimanjaro.
Gardner amefariki dunia jana Aprili 20, 2024 saa 11 alfajiri katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKIC) jijini Dar es Salaam alipokuwa anapatiwa matibabu.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo, leo Aprili 21, 2024 mwili wa Gardner utapelekwa nyumbani kwake Kijitonyama saa 12.00 jioni ambako kutakuwa na ibada ya faraja kwa familia.
Kesho Aprili 22, 2024 saa mbili asubuhi mwili utapelekwa katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Mbezi kwa ajili ya ibada.
Baadaye ya ibada mwili huo utapelekwa kwenye viwanja vya LeadersClub vilivyopo Kinondoni kwa ajili ya umma kutapata nafasi ya kushiriki kutoa heshima za mwisho.