pmbet

Gamondi aahidi pira burudani Moro

Sisti Herman

February 16, 2024
Share :

Kocha mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema wanaamini mchezo dhidi ya KMC utakaochezwa uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro utakuwa mgumu licha wao kupenda kucheza soka la kuburudisha.

 

“Mara zote huwa nasema napenda kucheza mchezo wa kuburudisha lakini naimani hautakuwa mchezo rahisi na sisi tupo hapa kwaajili ya kufanya vizuri ili kutimiza malengo yetu” Miguel Gamondi - Kocha Mkuu Young Africans SC 

 

Pia beki wa kushoto wa timu hiyo Nickson Kibabage amebainisha kuwa hii ni raundi ya maamuzi kwenye malengo ya msimu na namna pekee ni kushinda mchezo wa kesho.

 

“Raundi ya pili huwa ni ngumu lakini kwa ukubwa wa klabu ya Yanga tunahitaji kushinda kila mechi, sisi wachezaji kila sehemu tunayokwenda huwa tunatambua umuhimu wa mechi na tunaamimi kwenye kuwapa furaha mashabiki wetu" Nickson Kibabage Mchezaji wa Young Africans SC.

 

Gamondi na Kibabage wameyasema hayo kwenye mkutano wa waandishi wa habari kuelekea mchezo wa ligi kuu ya NBC dhidi ya KMC utakaopigwa kesho saa 10 jioni kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet