Gamondi achezwa na machale, kuifanyia kazi safu yake ya ulinzi
Eric Buyanza
February 15, 2024
Share :
Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi, ameonekana kushtushwa na kasi ya Simba katika mechi za hivi karibuni, hivyo ameanza kufanyia kazi safu yake ya ulinzi ambayo imekuwa ikiruhusu nyavu zao kutikiswa katika mechi mbili zilizopita.
Katika mbio hizo za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, Gamondi amesema inabidi afanye kazi ya ziada katika safu yake ya ulinzi, kwa kuwa timu wanayokimbizana nayo [Simba], inaonekana kiwango chao kuwa juu baada ya mapumziko ya mwezi mmoja na usajili mpya uliofanywa na 'Wekundu wa Msimbazi'.
Kikosi cha Yanga kimerejea jijini Dar es Salaam baada ya kumalizana na Tanzania Prisons kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya, hiyo ikiwa ni mechi ya pili kuruhusu bao.