pmbet

Gamondi alia na Diarra, Aziz Ki kutorejea wakiwakosa watano, Aucho, Yao na Pacome watajwa

Sisti Herman

March 29, 2024
Share :

Kocha mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema kuna uwezekano wa kuwakosa wachezaji muhimu wa kikosi cha kwanza dhidi ya Mamelodi Sundwons kwasababu kipa wak namba moja Djigui Diarra na Mfungaji wake kinara Stephanie Aziz Ki bado hawajajiunga na timu huku akiwa na rundo la majeruhi kikosini.

"Bado sijawaona Aziz Ki na Diarra walitarajiwa kurudi leo kutoka kwenye majukumu ya timu ya taifa.

"Lakini natarajia kuwakosa wachezaji wanne mpaka watano kutokana na majeraha ambayo waliyapata.

"Wachezaji kama Aucho,Yao na Pacome ni majeruhi bila kumsahau kibwana Shomari hii inatupa ugumu katika maandalizi ya mchezo wetu na Mamelodi kulingana n hali ya kikosi," 

Gamondi ameyasema hayo leo kwenye mkutano na wanahabari kwaajili ya mchezo wa robo fainali wa ligi yta mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundwons.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet