Gamondi alia na Rariba Yanga ikiwavaa Coastal
Sisti Herman
April 26, 2024
Share :
Kuelekea mchezo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya klabu ya Coastal Union kutokea Tanga, Kocha mkuu ameendelea kutoridhishwa na namna ratiba ya ligi ilivyo ngumu kwa michezo kufululizana ndani ya muda mfupi.
“Mechi zinapokuwa karibu sana muda wa maandalizi unakuwa mdogo, jana tumefanya mazoezi ya kurejesha miili sawa kwa Wachezaji na leo tutapata muda kidogo wa kujiandaa kwa ajili ya mchezo wa kesho na hapo ndipo nitajua Wachezaji wa kuwatumia"
"Mchezo wa kesho unahitaji sana ubora wa Wachezaji na angalau tunaenda kucheza kwenye Uwanja wenye mazingira mazuri, muhimu zaidi kesho ni kuweka mpira wavuni na kuibuka na ushindi” alisema Miguel Gamondi kocha mkuu wa klabu ya Yanga.
Gamondi ameyasema hayo kwenye mkutano na wanahabari leo kuelekea mchezo huo wa kesho utakaochezwa kwenye dimba la Azam Complex Chamazi kuanzia saa 12 jioni.