pmbet

Gamondi alia na ratiba Yanga ikiwavaa JKT leo

Sisti Herman

April 23, 2024
Share :

Ikiwa ni siku 2 tu kupita baada ya 'kuwanyoa' 2-0 watani zao Simba, klabu ya Yanga leo jioni itashuka kwenye dimba la Meja Jen. Isamuhyo Mbweni jijini Dar es Salaam kuwavaa klabu ya JKT Tanzania kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara huku kocha wao Mkuu Miguel Gamondi akionyesha kutoridhishwa na namna ratiba zilivyo kwa upande wao.

"Siwezi kuongea sana kuhusu maandalizi yetu dhidi ya JKT Tanzania, maana tulicheza jumamosi na jumapili wachezaji walikuwa na mapumziko leo (jana) ndio tumefanya mazoezi tumejaribu kufanya vizuri zaidi kwa ajili ya mechi yetu ya kesho (leo)" alisema Miguel Gamondi jana kwenye mkutano na wanahabari.

Yanga wanaoongoza msimamo wa ligi watachuana na JKT iliyopo nafasi YA 15 kati ya timu 16.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet