pmbet

Gareth Bale aliichomolea Man Utd

Eric Buyanza

March 5, 2026
Share :

Gareth Bale amethibitisha kuwa Manchester United ilitaka kumsaini kutoka Tottenham Hotspur kabla hajajiunga na Real Madrid kwa rekodi ya dunia mwaka 2013.


Bale anasema alikuwa na mazungumzo na Man Utd, lakini aliamua kujiunga na Madrid kwa sababu ya changamoto mpya na fursa ya kufanya kazi na kocha Carlo Ancelotti.


Man United, ambao walikuwa wamemteua David Moyes kama mrithi wa Sir Alex Ferguson, walikuwa na hamu ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 wakati huo, lakini walishindwa na miamba ya Uhispania Real Madrid, ambao walilipa pauni milioni 85 na kumpa mshambuliaji huyo mkataba wa miaka sita.

Bale aliendelea kufurahia maisha yake ya miaka tisa akiwa Bernabeu, akishinda Ligi ya Mabingwa mara tano, mataji matatu ya La Liga, Copa del Rey moja na mataji matatu ya Kombe la Dunia la Klabu la FIFA.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet