Gauni la marehemu lauzwa kwa Shilingi Bilioni 2.8
Eric Buyanza
December 21, 2023
Share :
Gauni lililovaliwa na marehemu Princes Diana, Binti mfalme wa Wales mnamo mwaka 1985 imeuzwa kwenye mnada kwa bei iliyokadiriwa kuwa mara 11 zaidi ya bei halisi.
Gauni hilo la velvet nyeusi, liliuzwa kwa pauni laki 9 (sawa Bilioni 2.8 za kitanzania) katika mnada wa Julien's Auctions mjini Hollywood.
Gauni hilo limeweka rekodi mpya ya ulimwengu kwa kuwa vazi ghali zaidi la Princess Diana kuwahi kuuzwa.
Diana alivaa vazi hilo kwa mara ya kwanza mjini Florence, Italia mnamo 1985 kwenye dhifa ya chakula cha jioni akiwa kwenye ziara ya kifalme na mume wake wa wakati huo Mwanamfalme Charles, Mtawala wa Wales, na tena kwenye Orchestra ya Vancouver Symphony mnamo 1986.