pmbet

Gaye: AFCON 2027 isipelekwe Afrika Mashariki hakuna hata barabara

Sisti Herman

January 18, 2026
Share :

 

Mwanahabari wa Ivory Coast, Mamadou Gaye amefanya mashambulizi makali dhidi ya nchi tatu za Afrika Mashariki (Kenya, Tanzania na Uganda) zinazotarajiwa kuandaa michuano ya kombe la mataifa ya afrika AFCON 2027, akiweka shaka juu ya uwezo wao wa kufikia viwango vya michuano hiyo.

“Inayofuata (AFCON) inaelekea nchi 3 za Afrika Mashariki ambako tayari nimefika, hakuna barabara ndani ya nchi, baadhi ya wenzangu kutoka Afrika Mashariki waliniambia kutoka nchi moja hadi nyingine itakuchukua siku 2 kuendesha gari"

"Halafu wasiwasi wangu mkubwa, na wengi wana wasiwasi, je tutashusha viwango kwa kwenda Afrika Mashariki, suluhu ni nini mbele?"

Hizi zilikuwa sehemu ya nukuu zake wakati wa mkutano wa Rais wa CAF Patrice Motsepe na waandishi.

Je, kuna uwezekano wowote kwamba itaondolewa katika nchi hizo?.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet