pmbet

GB 64 wa Simba akamatwa na Polisi

Sisti Herman

April 19, 2024
Share :

Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Jumanne Murilo amemethibitisha jeshi hilo kumkamata shabiki maarufu wa klabu ya Simba Abdulshahib Hegga GB 64 kwa tuhuma za kuhamasisha watu kufanya vurugu katika mchezo wa dabi ya Kariakoo kati ya Yanga na Simba kupitia video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Jeshi la Polisi limethibitisha hayo kupitia taarifa waliyoitoa kwa vyombo vya habari Leo tarehe 19.04.2024.

"Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linafuatilia kwa ukaribu mchezo wa soka siku ya jumamosi tarehe 20.04.2024 saa 11 jioni kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.Mchezo huo ni wa watani wa jadi kati ya klabu ya Simba na klabu Simba zote za Dar es Salaam na utakaochezwa.

"Kuelekea mchezo huo,Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limechukua tahadhari za kiusalama kabisa, wakati na baada ya mchezo.Usalama siku ya mchezo utakuwa wa kiwango cha juu,maeneo yanayozunguka uwanja ndani,nje na barabara za kuingia na kutoka uwanjani ukaguzi utakuwa wa hali ya juu kabla ya kuingia uwanjani,Hairuhusiwi mtu yeyote kwenda uwanjani na silaha ya aina yoyote, isipokuwa baadhi ya vyombo vya dola vyenye jukumu la usalama wa eneo hilo.

"Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemkamata Abdulshahib Hegga GB 64 kwa tuhuma za kuhamasisha watu kufanya vurugu katika mchezo huo kupitia kipande cha video alichokisambaza kwenye mitandao ya kijamii. Mtuhumiwa huyo anahojiwa kwa kina".

Ilisema taarifa hiyo kwa umma kuelekea mchezo huo.

Kabla ya taarifa hiyo kwa umma shabiki huyo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii alichapisha video akielezea kwa ufupi kinachoendelea akiripoti polisi huku akisikika akisema "Maneno yameniponza"

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet