Geay ashinda medali ya dhahabu Daegu Marathon kwa mara ya pili mfululizo
Sisti Herman
February 22, 2026
Share :

Baada ya nyota wa mbio za marathoni kutoka Tanzania, Gabriel Geay, kumaliza wa kwanza katika mbio za Daegu Marathon nchini Korea Kusini mwaka jana Februari 23, 2025 akimaliza kwa saa 2:05:22, nyota huyo amefanikiwa tena kutetea medali yake baada ya kumaliza wa kwanza tena katika mbio za Daegu Marathon za mwaka 2026.
Mwaka uliopita Geay alionyesha kiwango kikubwa cha ushindani na kufanikiwa kutwaa medali ya dhahabu akimzidi Addisu Gobena wa Ethiopia, jambo ambalo limezidi kuimarisha wasifu wake kama mmoja wa wakimbiaji bora wa masafa marefu duniani.
Geay ndiye Mtanzania anayeshika rekodi ya kukimbia mbio ndefu kwa muda mfupi zaidi aliyoiweka mwaka 2023 kwenye Boston Marathon akikimbia kwa saa 2:03:00, mwaka huu amemaliza kwa saa 2:08:04.





